Skip to main content

JEDWALI LA IPA NA DHANA YA UGHUNI


Na Mustafa H. Piku Malibiche
Karibuni wasomaji wetu katika somo la Kiswahili. Leo tutatoa ufafanuzi wa maswali mawili ambayo ni: 
MASWALI:
1.      Kwa kutumia jedwal la sauti IPA, kueleza dhana ya ughuni na sighuna ukihusisha mahali na jinsi ya matamshi ya konsonanti zisizopungua kumi.
2.      Kwa kutumia mifano mbalimbali, eleza mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika kuunda maneno ya lugha. Mifano iwe ya kitabuni na isiyo ya kitabuni.

SWALI LA I -MAJIBU
Majibu ya swali hili yamegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni utangulizi unaoelezea maana ya jedwali la sauti (IPA), maana ya dhana ya ughuni na si ghuna na konsonanti.Sehemu ya pili ni kuhusisha ughuni na sighuni na mahali na jinsi ya matamshi ya konsonanti na mwisho ni hitimisho.
Jedwali la herufi za konsonanti (IPA) linaelezea mahali pa matamshi, jinsi matamshi yanavyofanyika na hali ya ughuna au si ghuna wa konsonanti husika (Roach, 1997, Uk.19).
Ughuni unaelezewa kuwa ni hali ya utoaji wa sauti inayotokana na mtetemo wakati wa matamshi ya herufi za konsonanti, utamkaji ambao husababishwa na hewa itokayo kwenye mapafu kubanwa na ala za sauti kuachiwa na kusababisha mtetemo wakati wa kutamka baadhi ya sauti. Si-ghuna inaelezwa kuwa ni uhafifu wa sauti za herufi za konsonanti unaosababishwa na kuzuiwa na kuachiwa ghafla kwa hewa wakati wa utamkaji wa baadhi ya konsonanti na hivyo kutokuwa na mtetemo wa ala za sauti (Roach, 1997, Uk 31)
Konsonanti ni foni au herufi ambazo wakati wa kutamka kwake hewa hutatizwa kwa namna fulani, wakati mwingine hewa huzuiwa na wakati mwingine hutatizwa kiasi au kubanwa kiasi baada ya kupitia koromeo.
Uainishwaji wa Konsonanti katika jedwali la IPA unathibitisha aina kuu sita za sifa za konsonanti kwa makundi kama ilivyoelezwa  na Masamba na wenzake (2006) na Mgulu (1999) na Taasisi ya Ukuzaji mitaala Tanzania (1992, Uk. 63) kama ifuatavyo: vizuiwa/vipasuo, vikwamizi, vizuiwa-kwamizi, vimadende, nazali (ving’ong’o) na Vitambaza.
Vipasuo (vizuiwa) ni konsonanti ambazo hutokea wakati hewa ya mapafuni hupitia chemba ya mdomo na kubanwa kabisa na kuachiwa ghafla na kusababisha mlipuko unaosababisha utokeaji wa sauti hafifu na zenye mtetemo. Vipasuo ghuna ni [p] hutokea baada ya kukutana kwa midomo yote miwili, [d] hutokea wakati ncha ya ulimi inapokutana na ufizi wa juu, [g] hutokea baina ya kiganja cha ulimi kinavyokutana na kaakaa laini ambavyo uhusishwa na kubanwa kwa hewa na kuachiwa kwa ghafla na kusababisha utokeaji wa  mrindimo wa sauti (nyuzi za sauti).
Nyongeza ya hapo pia kuna vizuiwa ambavyo ni si-ghuna ambavyo ni [p] ambayo hutokea baadaya midomo miwili kuzuia hewa  itokayo mapafuni na kuachia mpenyo ghafla na kuruhusu mpasuko wa hewa, [t] ambayo hutokea baina ya ufizi na ncha ya ulimi, na [k] ambayo kinachotokea baina ya sehemu ya nyuma ya ulimi inapokwamiza hewa  katika kaakaa laini na kuachia hewa kwa ukakasi.
Vikwamizi, hutokana na kukwamizwa kwa hewa na ulimi katika kaakaa gumu. Sauti hizi hutamkwa pale ambapo ala za matamshi huwa zinakaribiana na kusababisha hewa inayopita toka mapafuni kukwaruza ala za sauti. Vikwamizi hivyo ni [v], [z], [j], ambavyo ni ghuna na [Ѳ], [f], [s], [ᵭ] na [h] ambavyo ni so-ghuna. Vikwamizi ghuna [v] hutokea wakati midomo ya chini inapokutana na meno ya juu, [z] hutokea wakati ala sogezi ya ulimi inaposogelea katika ufizi na kusabaisha kukwamizwa kwa hewa na kuzaa sauti mtetemo, na [j] hutokea wakati sehemu ya juu ya ulimi inaposogelea kaakaa gumu na kukwamiza hewa itokayo mapafuni.
Nyongeza ya hapo ni kwamba; Vikwamizi so ghuna  kwa mfano [f] hutokea wakati midomo ya chini inaposogeleana na meno ya juu na kukwamiza hewa itokayo mapafuni na hewa hiyo kuachiwa ghafla , [s] hutokea kwenye ufizi kutokana na hewa kutoka mapafuni kuruhusiwa kutoka nje wakati ulimi umerudi nyuma na kuachia mwanya wa hewa kupita, [ᵭ] hutokea kwenye meno yanapo na ulimi na kusababisha hewa itokayo mapafuni kukwamizwa na ikiachiwa huku ikitetema na kutoa sauti n.k.
Vizuiwa-kwamizi, hutokea wakati hewa inazuiwa na kusukumwa nje kwa nguvu katika ala za kutamkia ambapo nafasi ndogo huachiwa ili kuruhusu hewa chache kupita ikiwa na mkwaruzo.Sauti hizo ni [   ] [    ] ambazo ni ghuna hutokea katika kaakaa gumu na [ ʧ ],[č] ambazo ni so-ghuna
Kimadende ni sifa ya konsonanti ambayo hutokea inayotokea wakati wa kupigwapigwa kwa ulimi kwenye ufizi. konsonanti [r] ni ghuna mfano wa sauti ya neno /refu/.
Nazali (ving’ong’o) navyo vyaweza kuwa ghuna na so ghuna.Mfano wa sauti hizo ni [m], [n], na [ŋ].Konsonanti hizo hutokea kwa kuhusishwa kimio na na hewa kutoka mapafuni huelekezwa kupitia chemba ya pua ambapo hewa huzuiwa katika sehemu mbalimbali za chemba ya kinywa na kuruhusu ipitie katika chemba ya pua. Herufi [m] ni ghuna inayohusisha hewa kuzuiwa na mdomo, [n] ni ghuna inayohusisha hewa kuzuiwa na ulimi, [ŋ] inayohusisha hewa kuzuiwa kwenye kaakaa laini.
Vitambaza ni konsonanti ambayo ni kitambaza [l] ambayo ni ghuna inayotokea wakati sehemu ya kati ya ulimi  inapogusana na kaakaa gumu na kuacha nafasi ndogo ya hewa kupita ikisababisha mkwaruzo ambao si mkubwa sana. Hewa hiyo husukumwa nje, kuzuiwa na kuruhusiwa kupita pembeni mwa kizuizi ambacho ni ulimi.
Tunaweza kuhitimisha kuwa b, d, g, j, l, m, n, r. na t ni herufi ambazo zimeelezewa katika dhana ya ughuni na p, f, k, na t katika dhana ya si-ghuni kama ilivyoelezwa katika jedwali la IPA namna ambavyo sauti hizo hutokea.

REJEA
1.      Massamba, D.P.B., Y.M. Kihore na Y.P. Msanjila (2004). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu   
                        (FOKISA): Sekondari na Vyuo, Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa 
                         Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
2.      Mgullu, R.S. (1999). Mtaala wa Isimu: Fonetiki na Fonolojia ya Kiswahili. Nairobi:
                         Longhorn Publishers.
3.      Roach, P.(1997). English Phonetics and Phonology. Second Edition- A self-Contained   
                       Comprehensive Pronunciation Course. Cambridge University Press.
4.      Maganga.C, Mbunda. F.L., na wenzake (1993).Kiswahili Vyuoni. Taasisi ya Ukuzaji Mitaala             
                       Tanzania.KIUTA-NPC-Dar es Salaam


 SWALI LA II-MAJIBU

Kuundwa kwa maneno ya lugha ni dhana ya inayoashiria kukua kwa msamiati na matumizi ya lugha hiyo. Kwa maana nyingine, ni kupanuka kwa matumizi ya lugha. Mbinu rahisi inayotumika katika kuunda maneno ya Lugha ya Kiswahili ni pamoja na kukopa maneno toka lugha nyingine mfano; Kiswahili kukopa baadhi ya maneno kutoka kiarabu kama vile neno alasiri ( adhuhuri)
Zipo kanuni nyingi za uundaji wa maneno katika lugha. Baadhi ya njia/ mbinu zitumikazo katika uundaji wa maneno ya lugha ya Kiswahili ni: Uambishaji na unyumbuaji, uambatishaji, urudufishaji, akronimi na uhulutishaji na uundaji mpya wa maneno.
Uambishaji wa maneno unamaanisha ni tendo la kunyumbua baadhi ya maneno ya Kiswahili kwa kuambisha mofimu tangulizi na au mofimu fuatishi za neno hilo na hupewa maana tofauti na aghalabu huingizwa  kwenye kundi tofauti la maneno, kwa mfano neno      
         
         Hoja: hoji, hojaji, hojiwa
         Koma: Komesha, komoa
         Vuta: Vutia, vutisha, vutika
Mizizi ya maneno hayo yaweza kuwekewa mofimu tangulizi na mofimu fuatishi na kupata majina mengine toka katika neon la awali mfano:
         Gomb- gombana, gombanisha, ugomvi, mgombezi, magombano.
Njia ya pili ni uambatishaji. Njia hii uhusika na uwekaji pamoja wa maneno mawili au zaidi ili kuunda au kuzalisha neon jipya. Njia hii ni namna nyingine ya unyambulishaji. Mwambatishaji maneno, badala ya kunyambua mofimu katika mzizi, huweka maneno mawili au zaidi pamoja. Maneno haya yanaweza kuwa huru au kuambatishwa na kunyambulishwa na mofimu. Kwa mfano;
         -askari+kanzu          askarikanzu
         -njugu+mawe          njugumawe
         -kesho+kutwa         keshokutwa
         -kiberiti+ ngoma        kiberitingoma
          -kiangaza+macho      kiangazamacho
          -kisima+mama        kisimamama
Uambataji huu wa maneno huunda/huibua fasili ya upamoja wa neon linalopatikana. Hii ina maanisha kuwa kwa mfano fasili ya askari+ kanzu pekee hupoteza uhusiano wa maana ya askari kanzu. Maana ya kila neno pekee hutofautiana katika neon lililoundwa.
Njia ya tatu ni urudufishaji.Katika njia hii, uundaji wa maneno hufanywa kwa urudufu ambapo maneno au sehemu ya neno hurudiwarudiwa. Urudufishaji wa neon zima ni urufishaji kamili na urudufu sehemu ya neon huitwa nusu rudufu. Kwa mfano:
        -bara+bara=barabara
        -nungu+nungu=Nungunungu
        -Ki+wili-wili=kiwiliwili
        -Ki+nyevu+nyevu= kinyevunyevu
Katika uundaji huu wa urudufu una msingi uliosawa. Maana ya neon moja hailingani na maana ya maneno mawili yanayoletwa pamoja. Mfano:
        -bara- nchi kavu
        -barabara- haimaanishi nchi kavu bali hubeba maana nyingine tofauti
                          -mbali na pwani
                          -pande mojawapo ya nchi kavu kumbe maana sahihi ni ya njia ndefu au njia kuu.
Njia/mbinu ya nne ni Akronimi na uhulutishaji. Njia hii hufupisha maneno yanayotumiwa kwa pamoja kwa kuchukua herufi za mwanzo tu maneno hayo mfano kutoka lugha ya kiingereza ni neno “NATO-North Atlantic Treaty Organization”. Katika lugha ya Kiswahili maneno kama:
        -UKIMWI-Upungufu wa Kinga Mwilini
        -TUKI-Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
        -BAKWATA-Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania
        -BAKITA- Baraza la Kiswahili la Taifa
        -BAWATA-Baraza la Wazee Tanzania
        -MKUZA-Mkakati wa Kupunguza Umaskini Zanzibar
Tendo hili huitwa Akronimi. Tendo jingine linalofanana na hili ni uhulutishaji (blending). Ni tendo linaloweka pamoja baadhi ya vijisehemu vya maneno ili kuunda neno jipya. Mfano:
        -Chakula cha jioni- chajio
        -Hati za kukataza- Hataza
        -Hati za kupunguza-hakuza
Njia ya tano ni uundaji wa maneno mapya. Njia hii uhusisha mawazo mapya  na kupewa majinaili kuleta dhana fulani mpya. Utaratibu wake  huanza kuchunguzwa uasili wa lugha za asili kuona maneno yabebayo dhana husika. Mfano:
a.       Ngeli: (Kihaya) likimaanisha aina ya vitu kuonesha majina
b.      Ikulu: (Kinyamwezi)-likimaanisha maskani/ nafasi ya mkuu wa nchi/ temi za wanyamwezi
c.       Beberu: Dume la mbuzi (maana ya asili), mtu aaminiye na kutetea siasa za ubeberu (utumiaji wa nguvu)-maana mpya.
Neno likikosa uasili toka katika makabila, huangaliwa lugha nyingine za kigeni na kurekebishwa kifonolojia na kimofolojia ili yaafikiane na kanuni za lugha ya Kiswahili kwa kuzingatia kanuni za mfuatano wa fonimu kwa mfano:
         KIKI- Konsonanti, irabu, konsonanti, irabu
         KIIKI- Konsonanti, irabu, irabu, konsonanti, irabu
         KIKKI- Konsonanti, irabu, konsonanti, konsonanti, irabu. Mfano ”shirt”-shati, “bicycle”-    
            Baiskeli, “bible” –biblia
Endapo inatokea neno la lugha nyingine kukosekana kupatikana basi neno jipya huundwa. Mfano: Ukarabati, Ukarafati, Kongamano, warsha.Uuundaji wa maneno huzingatia kanuni mbalimbali mfano, uambishaji na unyambuaji kama vile soma- m-som-i,u-som-i.Mchezo-m-chez-o, m-chez-aji.
Ili kuhitimisha, Njia hizi zote zimeelezwa kuwa na taratibu za kisayansi ya lugha ambazo hufuatwa ili kuleta ulinganisho na upatanisho wa kisarufi wa maneno husika ambayo huzaa sentensi.Hivyo basi uundwaji wa maneno hutumia njia nyingi kati ya hizo zilizotajwa ambazo ni


REJEA
Maganga.C.,Mbunda. F.L., na wenzake (1993).Kiswahili Vyuoni. Taasisi ya Ukuzaji Mitaala             
                      Tanzania.KIUTA-NPC-Dar es Salaam






























Comments

Popular posts from this blog

INVESTIGATING THE INFLUENCE OF LITERACY RICH CLASSROOM ENVIRONMENT ON LEARNING: A CASE STUDY OF ONE PRE AND LOWER PRIMARY SCHOOL IN NACHINGWEA DISTRICT, SOUTHERN TANZANIA MUSTAFA H. MALIBICHE

THE AGA KHAN UNIVERSITY TANZANIA INSTITUTE FOR HIGHER EDUCATION INSTITUTE FOR EDUCATIONAL DEVELOPMENT EASTERN AFRICA INVESTIGATING THE INFLUENCE OF LITERACY RICH CLASSROOM ENVIRONMENT ON LEARNING: A CASE STUDY OF ONE PRE AND LOWER PRIMARY SCHOOL IN NACHINGWEA DISTRICT, SOUTHERN TANZANIA MUSTAFA H. MALIBICHE A DISSERTATION SUBMITTED TO THE INSTITUTE FOR EDUCATIONAL DEVELOPMENT EASTERN AFRICA IN PARTIAL FULFILLMENT OF THE REQUIREMENT FOR THE COMPLETION OF MASTERS DEGREE IN EDUCATION (LANGUAGE AND LITERACY) DAR ES SALAAM – TANZANIA 27 th ,11, 2015 APPROVAL PAGE THE AGA KHAN UNIVERSITY Tanzania Institute for Higher Education Institute for Educational Development Eastern Africa TO: THE INSTITUTE FOR EDUCATIONAL DEVELOPMENT, EASTERN AFRICA MUSTAFA HAMISI MALIBICHE Full Name of Student I hereby give my permission for the research project of the above named student, for whom I have been acting as supervisor, to proceed to examination....