Na Mustafa H. Piku Malibiche Karibuni wasomaji wetu katika somo la Kiswahili. Leo tutatoa ufafanuzi wa maswali mawili ambayo ni: MASWALI: 1. Kwa kutumia jedwal la sauti IPA, kueleza dhana ya ughuni na sighuna ukihusisha mahali na jinsi ya matamshi ya konsonanti zisizopungua kumi. 2. Kwa kutumia mifano mbalimbali, eleza mbinu mbalimbali zinazoweza kutumika kuunda maneno ya lugha. Mifano iwe ya kitabuni na isiyo ya kitabuni. SWALI LA I -MAJIBU Majibu ya swali hili yamegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni utangulizi unaoelezea maana ya jedwali la sauti (IPA), maana ya dhana ya ughuni na si ghuna na konsonanti.Sehemu ya pili ni kuhusisha ughuni na sighuni na mahali na jinsi ya matamshi ya konsonanti na mwisho ni hitimisho. Jedwali la herufi za konsonanti (IPA) linaelezea mahali pa matamshi, jinsi matamshi yanavyofanyika na hali ya ughuna au si ghuna wa konsonanti husika (Roach, 1997, Uk.19). Ughuni...